Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatullah Khamenei katika kikao hiki, ameainisha kuwa maandalizi ya vifaa vya kijeshi kwenye jeshi la ulinzi yanamaanisha kuimarisha uwezo wa kijeshi na kuboresha muundo wa shirika, taasisi na hali ya maisha ya watumishi hao, na akaongeza: Sambamba na maandalizi ya programu, kujiandaa kisaikolojia yaani imani katika lengo na jukumu lao pamoja na yakini katika uhalali wa njia wanayoifuata ni jambo muhimu mno, ambapo kuna jitihada zinazofanywa na adui ili kupotosha.
Yeye ametaja kuwa; uwepo wa uislamu na kujitegemea kwa mfumo wa kiislamu, ndio sababu iliyo muamsha adui dhidi yake, na akaongeza kusema: Kile kinachomfanya adui awe na tahadhari si jina la “Jamhuri ya Kiislamu,” bali ni ile nia na azma ya nchi kutaka kuwa ya kiislamu, huru, na yenye utambulisho, na kutoegemea kwa wengine kwa ajili ya heshima yake, ambacho ndicho kinachowatia hasira.
Kiongozi wa Mapinduzi akitolea mfano wa moja mwenendo wa kinafiki wa wenye nguvu duniani kuhusu kuhalalisha kwao kuwa na silaha za kisasa na za kutisha kabisa, huku wakipiga marufuku maendeleo ya kijeshi kwa wengine, amesema:
Yakini, imani, azma, ushujaa na kumtegemea Mwenyezi Mungu vinapaswa kuwa kwa kiwango cha juu ndani ya majeshi ya ulinzi, kwa sababu majeshi yaliyokuwa makubwa kwa sura lakini yakakosa sifa hizi katika historia, yameshindwa.
Yeye anaona kuwa kuhifadhi na kuinua hali ya kujiandaa kiprogramu katika jamii kunahitaji juhudi za taasisi mbalimbali, ikiwemo redio na televisheni ya taifa pamoja na vyombo vya uenezi, na akaongeza: Kwa bahati nzuri, leo hii nchi yetu si tu imepiga hatua kubwa mbele katika upande wa vifaa, bali pia katika upande wa kiprogramu imeendelea sana, ambapo mfano wake ni hamasa isiyoelezeka ya mamia na maelfu ya vijana waumini na wenye ari ya juu ya kujitokeza kwenye nyanja zinazohitaji mapambano.
Hadhrat Ayatullah Khamenei ametaja sababu zinazomtia hasira adui na kelele zao kwenye vyombo vya habari kuwa ni maendeleo yanayozidi kushamiri ndani ya Iran, na amesema: Wao huyawasilisha mambo ambayo ni ndoto zao kama habari na uhalisia, hali ambayo inapaswa kutengenezewa mpango na kukabiliwa nayo katika uenezi.
Yeye, huku akisisitiza kuwa Jamhuri ya kiislamu inasonga mbele kwa harakati na maendeleo mazuri, ameongeza: Ni kweli kwamba kuna matatizo fulani ya kiuchumi yanayoonekana wazi ambayo yanapaswa kutatuliwa, lakini haifai kuchanganya masuala hayo na kupuuza maendeleo makubwa ambayo hata maadui wanalazimika kuyasifu.
Maoni yako